Katika Swala ya Dhuhrain iliyoswaliwa katika Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni, Dar-es-salaam, Sheikh Dkt. Swaleh Maulid alisisitiza kuwa mwanamke katika Uislamu ana nafasi ya ibada, uwajibikaji na mchango mkubwa katika kujenga jamii yenye maadili na maadili mema.

12 Juni 2026 - 16:29

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Leo Ijumaa, tarehe 12/06/2026, Swala ya Adhuhuri na Alasiri (Dhuhrain) ilitekelezwa katika mazingira ya kiibada yaliyohudhuriwa na jumla ya Wanafunzi Wasichana 144 wa Hawzah ya Sayyidat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam - Tanzania.

Katika tukio hilo, Khutba ilitolewa na Sheikh Dkt. Swaleh Maulid, ambapo alizungumzia kuhusu nafasi ya mwanamke katika Uislamu kupitia mtazamo wa ibada, uwajibikaji na mchango wake katika kujenga jamii yenye maadili mema.

Sheikh Dkt. Swaleh alisisitiza kuwa Uislamu umempa mwanamke nafasi ya heshima na wajibu mkubwa katika familia na jamii, akibainisha kuwa mwanamke ana mchango muhimu katika malezi, uadilifu wa kijamii na kuimarisha maadili ya Kiislamu kupitia elimu na tabia njema.

Aidha, alieleza kuwa ibada na ucha-Mungu kwa mwanamke ni msingi wa kujenga jamii imara, huku akihimiza wanafunzi kuzingatia maadili ya Kiislamu na kutumia elimu yao katika kuleta manufaa kwa jamii.

Your Comment

You are replying to: .
captcha